MIKATABA YA SCAFF KIGOMA


MKATABA WA AJIRA YA WASHONAJI


Mshahara wa mwajiriwa: Kama mwajiriwa alidarizi nguo ila hakuifunga, analipwa asilimia 30 ya malipo ya ushonaji wa nguo hiyo. Kama mwajiriwa hakudarizi nguo lakini aliifunga, analipwa asilimia 10 ya malipo ya ushonaji wa nguo hiyo. Malipo ya ushonaji wa nguo na utendaji wa kazi zingine zote ni asilimia 40 ya malipo ya kazi. Mteja atakayeomba kwamba kazi za wateja wengine zisimamishwe ili kazi zake zifanywe kwa haraka, atalipa asilimia 80, 65 au 50 juu ya bei ya kawaida. Kwenye asilimia mia ya hii asilimia ya juu, mwajiriwa anapalipwa asilimia 50.

Mshahara wa siku zisizo za kazi: Kwa sababu mwajiriwa analipwa kwa asilimia ya kipato cha kazi zake, halipwi mshahara wa siku zisizo za kazi.

Makato ya akiba: Mwajiri hukata wahajiriwa wote asilimia 7 ya mshahara kila mara wahajiriwa wanapopokea mshahara. Makato hayo yanawekwa kwenye akaunti ya akiba ya wahajiriwa. Kila mwajiriwa ana haki ya kupewa pesa zake wakati wowote ule anazihitaji. Ila ni lazima kila mwajiriwa awe na angalau shilingi elfu thelathini (TZS 30 000) katika akaunti hii ya akiba. Yaani mwajiriwa hawezi kutoa pesa kwenye akaunti ya akiba ikiwa ana kiasi cha pesa shilingi elfu thelathini (TZS 30 000) au chini ya hicho kiasi. Siku mwajiriwa atakapoacha kazi, atapewa pesa zake zote alizowekeza kwenye akaunti ya akiba ya wahajiriwa.

Marekebisho ya mshahara: Ikiwa mwajiriwa amepokea mshahara mwingi katika mapokezi iliopita kuliko kiasi angepaswa kupokea, kiasi kilichozidi kitakatwa kwenye mshahara wa mapokezi ijayo. Pia ikiwa mwajiriwa amepokea mshahara mdogo katika mapokezi iliopita kuliko kiasi angepaswa kupokea, kiasi kilichokosa kitalipwa pamoja na mshahara wa mngao ujao.

Makato kwa ajili ya deni: Ikiwa mwajiriwa hakuheshimu tarehe ya mwisho ya ulipaji wa deni ambayo alikopa kwa mwajiri, atakuwa akikatwa kwenye mshahara wake hadi deni yote ilipwe.

Malipo ya hifadhi ya jamii na malipo mengine kwenye serikali au ofisi zingine: Mwajiri na mwajiriwa watalipa na kuhifadhi michango kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kama sheria inavyoelekeza. Malipo mengine ya serikali au ya ofisi zingine yatalipwa pia kama inavyoelekezwa na sheria. Malipo na michango ya mwajiriwa yanakatwa kwenye mshahara wa mwajiriwa. Malipo na michango ambayo mwajiri anatakiwa kulipa / kuchanga yatatolewa kwenye mfuko wa mwajiri.

Siku na saa za kazi: Siku na saa za kawaida za kazi ni Jumatatu, Jumanne, Jumatano, Alhamisi na Jumamosi saa 07:00 hadi saa 21:00. Saa ya mwisho mwajiriwa kufika kazini ni 09:00. Ila kama kuna siku ambazo mwajiri anahitaji mwajiriwa afike kazini kabla ya saa 09:00, ni lazima mwajiriwa atii mwajiri kama hakuna kizuizi chochote kama vile mangonjwa. Saa ya kwanza mwajiriwa anaweza toka kazini ni 19:00. Ila kama kuna siku ambazo mwajiri anahitaji mwajiriwa atoke kazini baada ya saa 19:00, ni lazima mwajiriwa atii mwajiri kama hakuna kizuizi chochote kama vile mangonjwa. Inakatazwa mwajiri kumlazimisha mwajiriwa kufanya kazi kabla ya saa za kufunguwa ofisi na baada ya saa za ofisi kufunga.

Kazi ya ziada: Mwajiriwa na mwajiri wanaweza kukubaliana kwamba mwajiriwa afanye kazi ya ziada. Saa za kazi ya ziada ni saa 06:00 hadi 06:59, na saa 21:01 hadi saa 23:00 katika siku za kawaida za kazi. Mwajiriwa anaweza pia kufanya kazi ya ziada Ijumaa au Jumapili ikiwa kuna makubaliano kati ya mwajiri na mwajiriwa. Hairuhusiwi kuanza kazi mapema kuliko saa 09:00 siku kama hiyo. Pia hairuhusiwi kumaliza kazi baadaye kuliko saa 19:00 siku kama hiyo. Inakatazwa kufanya kazi ya ziada siku zote mbili za mapumziko ya wiki. Mkataba huu unakataza mwajiri kumlazimisha mwajiriwa kufanya kazi ya ziada kama mwajiriwa hataki. Mkataba huu unakataza pia mwajiriwa kufanya kazi ya ziada bila makubaliano na mwajiri.

Kutoa taarifa ya kutokufika au kuchelewa kazini: Ikiwa mwajiriwa hawezifika kazini kwa muda kama vile mkataba huu unavyoelekeza, lazima amtaarifu mwajiri haraka, mwisho masaa 2 kabla ya saa ambayo mwajiriwa atakuwa ayupo kazini. Mwajiriwa anataarifu kupitia simu, kwa kutuma ujumbe na mtu au kwa kujitokeza ofisini. Ikiwa mwajiriwa anazuiwa kutaarifu kwa sababu ya ukosefu wa simu au mjumbe, au hana namna ya kufika ofisini, lazima atowe sababu ya kutokufika kazini ndani ya masaa 24. Masaa yanaesabiwa kwa kuanzia saa ya mwisho ambayo mwajiriwa angekuwa kazini. Isipokuwa tu kama mwajiriwa anaumwa sana au amepatwa na hali ngumu kama vile kilio au ajali. Katika hali kama hizo, bado mwajiriwa analazimika kumtaarifu mwajiri haraka iwezekanavyo, lakini hakuna muda wa mwisho wa kutaarifu.

Saa za mapumziko: Mwajiriwa atakuwa na mapumziko ya dakika 120 kwa siku. Mwajiri atakubaliana na mwajiriwa kuhusu wakati wa mapumziko. Kama hakuna makubaliano yo yote yale au kama mwajiriwa na mwajiri wameshindwa kukubaliana kuhusu wakati wa mapumziko, mwajiriwa atakuwa na mapumziko saa 13:00 hadi saa 15:00.

Likizo ya sikukuu: Mwajiriwa ana haki ya siku 20 kwa mwaka za sikukuu za umma, taifa na za kidini.

Likizo ya mwaka: Mwajiriwa ana haki ya siku 32 za likizo ya mwaka. Mwajiri anaweza kataa pendekezo la mwajiriwa kuhusu kipindi na siku za likizo, ila ni lazima mwajiri atowe sababu halali. Kama hakuna makubaliano yoyote yale au kama mwajiriwa na mwajiri wameshindwa kukubaliana kuhusu kipindi cha likizo ya mwaka, mwajiriwa atakuwa na likizo ya mwaka ya siku zisizopungua 21 (kuanza tarehe moja hadi tarehe ishirini na moja mwezi wa saba). Mwajiriwa mpya ambaye hajafanya kazi kwa miezi 12 hawezi kulazimishwa kuchukua likizo. Anachukuwa likizo tu ikiwa anataka mwenyewe.

Likizo ya ugonjwa: Mwajiriwa ana haki ya likizo ya ugonjwa ya siku 28 kwa mwaka bila kuonyesha kithibitisho kutoka kwa daktari. Baada ya hizo siku 28, mwajiriwa anapaswa kuwa na kithibitisho kutoka kwa daktari kila mara anapodai ni mgonjwa. Ikiwa utakuwa ugonjwa wa muda mrefu, mwajiriwa anapaswa kuleta kithibitsho mpya kutoka kwa daktari kila mwezi.

Likizo ya uzazi: Mwajiriwa ana haki ya siku 300 za likizo ya uzazi kama ni yeye ndiye mtu wa karibu sana kwa mtoto kimalezi. Mwajiriwa ana haki ya siku 90 za likizo ya uzazi kama si yeye ndiye mtu wa karibu sana wa mtoto kimalezi.

Likizo zingine muhimu: Mwajiriwa ana haki ya siku 21 kwa mwaka kwa ajili ya mambo mengine muhimu, kwa mfano magonjwa katika familia na sherehe za arusi.

Kutoa taarifa ya likizo: Mwajiriwa analazimika kutoa taarifa ya likizo mapema sana, mwisho siku thelathini (30) kabla ya likizo.

Mengineyo: Mwajiriwa anastahili kupata haki zote za msingi kama inavyoelekeza sheria. Haki, kanuni na maslahi mengine au ulinzi ambao anastahili mwajiriwa ni sehemu ya mkataba huu hata kama haziandikwi kwenye mkataba.

Mwanzo na mwisho wa mkataba: Mkataba una tarehe ya kuanza, na unaendelea hadi upande mmoja utakapoamua kuhusitisha. Upande utakaoamua kusitisha mkataba, utajulisha upande mwingine siku 30 kabla ya tarehe ambazo kazi itasimamishwa. Makubaliano katika mkataba huu yanaendelea hadi tarehe ambayo kazi itasimamishwa. Upande utakao simamisha kazi kabla ya siku 30 hazijapita toka tarehe ya taarifa ya usitishaji wa kazi, utalipa faini ya shilingi elfu thelathini (TZS 30 000) kwenye upande mwingine. Kwa upande wa mwajiriwa, pesa zinaweza kukatwa kwenye mshahara wake au kwenye akaunti ya kiba. Faini hailipwi kama ni upande unao dai faini ndoo uliosababisha upande mwingine kusimamisha kazi mapema.

Kipindi cha majaribio: Kipindi cha majaribio ni siku 30. Katika kipindi cha majaribio mwajiriwa anaweza kuachishwa kazi wakati wowote ule kama hafanyi kazi istahilivyo. Kama mwajiriwa anaweza kufanya kazi istahilivyo, lakini ukosefu wa mafunzo kuhusu vifaa vya kazi na miongozo ya kazi ndoo unasababisha kazi kufanyika vibaya, mwajiri hana haki ya kumuachisha mwajiriwa kazi.

MKATABA WA UJIFUNZAJI

Siku na saa za mafunzo: Siku na saa za mafunzo ni Jumatatu, Jumanne, Jumatano, Alhamisi na Jumamosi saa 08:30 hadi saa 18:30. Mkataba huu unakataza mwanafunzi kufanya kazi au mafunzo ya ziada.

Kutoa taarifa ya kutokufika au kuchelewa kazini: Ikiwa mwanafunzi hawezifika kazini kwa muda kama vile mkataba huu unavyoelekeza, lazima amtaarifu fundi haraka, mwisho masaa 2 kabla ya saa ambayo mwanafunzi atakuwa ayupo kazini. Mwanafunzi anataarifu kupitia simu, kwa kutuma ujumbe na mtu au kwa kujitokeza ofisini. Ikiwa mwanafunzi anazuiwa kutaarifu kwa sababu ya ukosefu wa simu au mjumbe, au hana namna ya kufika ofisini, lazima atowe sababu ya kutokufika kazini ndani ya masaa 24. Masaa yanaesabiwa kwa kuanzia saa ya mwisho ambayo mwanafunzi angekuwa kazini. Isipokuwa kama mwanafunzi anaumwa sana au amepatwa na hali ngumu kama vile kilio au ajali. Katika hali kama hizo, bado mwanafunzi analazimika kumtaarifu fundi haraka iwezekanavyo, lakini hakuna muda wa mwisho wa kutaarifu.

Saa za mapumziko: Mwanafunzi atakuwa na mapumziko ya dakika 60 kwa siku. Fundi atakubaliana na mwanafunzi kuhusu wakati wa mapumziko. Kama hakuna makubaliano yo yote yale au kama mwanafunzi na fundi wameshindwa kukubaliana kuhusu wakati wa mapumziko, mwanafunzi atakuwa na mapumziko saa 13:00 hadi saa 14:00.

Likizo ya sikukuu: Mwanafunzi ana haki ya siku 20 kwa mwaka za sikukuu za umma, taifa na za kidini.

Likizo ya mwaka: Mwanafunzi ana haki ya siku 32 za likizo ya mwaka. Fundi anaweza kataa pendekezo la mwanafunzi kuhusu siku na kipindi cha likizo, ila ni lazima fundi atowe sababu halali. Kama hakuna makubaliano yoyote yale au kama mwanafunzi na fundi wameshindwa kukubaliana kuhusu kipindi cha likizo ya mwaka, mwanafunzi ana haki ya likizo ya mwaka ya siku zisizopungua 21 (kuanza tarehe moja hadi tarehe ishirini na moja mwezi wa saba). Mwanafunzi hawezi kulazimishwa kuchukua likizo. Anachukuwa likizo tu ikiwa anataka mwenyewe.

Likizo ya ugonjwa: Mwanafunzi ana haki ya likizo ya ugonjwa ya siku 28 kwa mwaka bila kuonyesha kithibitisho kutoka kwa daktari. Baada ya hizo siku 28, mwanafunzi anapaswa kuwa na kithibitisho kutoka kwa daktari kila mara anapodai ni mgonjwa. Ikiwa utakuwa ugonjwa wa muda mrefu, mwanafunzi anapaswa kuleta kithibitsho mpya kutoka kwa daktari kila mwezi.

Likizo ya uzazi: Mwanafunzi ana haki ya siku 300 za likizo ya uzazi kama ni yeye ndiye mtu wa karibu sana kwa mtoto kimalezi. Mwanafunzi ana haki ya siku 90 za likizo ya uzazi kama si yeye ndiye mtu wa karibu sana wa mtoto kimalezi.

Likizo zingine muhimu: Mwanafunzi ana haki ya siku 21 kwa mwaka kwa ajili ya mambo mengine muhimu, kwa mfano magonjwa katika familia na sherehe za arusi.

Kutoa taarifa ya likizo: Mwanafunzi analazimika kutoa taarifa ya likizo mapema sana, mwisho siku thelathini (30) kabla ya likizo.

Kuhusu mshahara: Mwanafunzi halipwi mshahara kwa kazi anazofanya. Kazi anazofanya zitakuwa zikisajiliwa kwa jina la mwalimu wake, yaani fundi. Wahajiriwa kawaida tu ndio wana haki ya mshahara.

Kuhusu kujeruhiwa au kuugua kazini: Mwanafunzi akijeruhiwa na vifaa vya kazi wakati wa kazi, utalipiwa gharama za matibabu na mwajiri wa fundi. Gharama ambazo hugharamiwa na mwajiri wa fundi ni gharama ambazo hazilipwi na serikali, vitengo vingine, shirika zingine au watu wengine. Mwajiri wa fundi hachukui jukumu la majeraha na magonjwa ambayo hayatokani na kazi, hata ikiwa jeraha au ugonjwa umetokea wakati wa saa za kazi. Ila ikiwa mwanafunzi ameugua au kujeruhiwa sana kiasi kwamba hawezi kwenda nyumbani, hospitalini au kwa daktari peke yake, mwajiri wa fundi atalipa gharama za kufikisha mwanafunzi nyumbani, hospitalini au kwa daktari hata kama ungonjwa au jeraha ahukusababishwa na kazi.

Mengineyo: Mwanafunzi anastahili kupata haki zote za msingi kama inavyoelekeza sheria. Haki, kanuni na maslahi mengine au ulinzi ambao anastahili mwanafunzi ni sehemu ya mkataba huu hata kama haziandikwi kwenye mkataba.

Mwanzo na mwisho wa mkataba: Mkataba una tarehe za kuanza na unaendelea hadi upande mmoja utakapoamua kuhusitisha. Pande zote zinaweza kusitisha mkataba huu wakati wowote ule.

Maelekezo ya kusaini mkataba: Ikiwa mwanafunzi yuko chini ya umri wa miaka 18, ni lazima mmoja kati ya wazazi wake asaini. Ikiwa mwanafunzi ana umri wa zaidi ya miaka 18, inatosha yeye tu asaini.


Ilisasishwa mwisho: 29.06.2022
Inatumika kutoka: 01.07.2022