SCAFF KIGOMA


MWONGOZO WA KAZI

1. Katika kazi za kibinafsi, kila mtu ana uwezo wa kujiamuliya mwenyewe masaa ya kazi na kanuni, sera, sheria na taratibu za utendaji wa kazi. Katika shirika, mtu hawezi kujiamulia mwenyewe. Shirika zote zina kanuni, sera, sheria na taratibu zao ambazo wafanyakazi wanalazimika kufuata na kuheshimu. Miongoni mwa mambo mengine, kanuni, sera, sheria na taratibu zinatengenezwa ili kila mtu atendewe sawa na kwa haki, na ili wamiliki na wasimamizi wa mashirika wasidhulumu wafanyakazi. Bila kanuni, sera, sheria na taratibu, hakuna shirika ambalo linaweza kusimama.

2. Mfanyakazi atakayevunja kanuni, sera, sheria na taratibu za kazi atapewa onyo na miongozo ya marekebisho mara tatu. Uvunjaji ukirudiliwa mara ya nne, mfanyakazi anahachishwa kazi. Mfanyakazi anaweza hachishwa kazi baada ya kufanya kosa mara moja tu kama kosa lililotendwa ni kubwa na linaweza leta hasara kwenye kazi. Mfano wa kosa kama hilo ni vitendo vya ngono, ghasia, vitisho vya ghasia, rushwa, ugonvi, wizi, kusema uwongo, kutukana, kusengenya au kukataa maagizo halali ya meneja.

3. Meneja anaruhusiwa kufanya maamuzi ya muda mfupi ikiwa kuna jambo, hali au tatizo limejitokeza ambalo linahitaji kuchukuliwa hatua au ufafanuzi ambao bado haujawa kwenye mwongozo huu. Lakini maamuzi ya meneja yatakuwa ni ya muda mfupi tu. Muda mfupi yaani kipindi kisichozidi masaa 48. Wakati jambo, hali au tatizo kama hilo linapotokea, ni lazima meneja awasiliane na wamiliki haraka iwezekanavyo ili hatua ichukuliwe kuhusu kanuni, sera, sheria au taratibu ambazo bado hazijawa kwenye mwongozo huu. Maamuzi ya meneja ahipaswi kusababisha ukiukaji wa haki za wafanyakazi na wateja, au uvunjaji wa sheria za inchi na miongozo katika mikataba ya ajira.

4. Meneja anaruhusiwa pia kuchukuwa maamuzi ya muda mfupi yasioambatana na mwongozo huu kama maamuzi hayo ya muda mfupi yatasababisha utendaji bora zaidi wa kazi au mapato mazuri zaidi. Lakini maamuzi ya meneja yatakuwa ni ya muda mfupi tu. Muda mfupi yaani kipindi kisichozidi masaa 48. Maamuzi ya meneja ahipaswi kusababisha ukiukaji wa haki za wafanyakazi na wateja, au uvunjaji wa sheria za inchi na miongozo katika mikataba ya ajira. Maamuzi ya muda mfupi yasioambatana na mwongozo huu ahirusiwi ikiwa yatasababisha matokeo mabaya katika kipato au utendaji wa kazi. Meneja analazimika kuripoti kwa wamiliki kila mara anapofanya maamuzi ya muda mfupi yasioambatana na mwongozo huu wa kazi.

5. Meneja anapaswa kuhusisha na kujulisha wamiliki kabla ya kuajiri au kuachisha mfanyakazi kazi. Meneja anapaswa pia kujulisha wamiliki kama kuna mfanyakazi ambaye amehacha kazi kwa hiyari yake. Wanafunzi huingia mikataba na waalimu wao, lakini walimu hawawezi kuingia mikataba au kuisitisha bila kumjulisha meneja.

6. Meneja ndiye msimamizi mkuu wa kazi zote na wafanyakazi wote. Inakatazwa kufanya kazi yoyote ofisini bila kumjulisha meneja. Wateja wanapokelewa na meneja, lakini wafanyakazi pia wanaweza kupokea wateja. Kabla ya mfanyakazi kuanza na utendaji wa kazi ambazo amepewa na mteja, ni lazima amjulishe meneja.

7. Kila mfanyakazi anaruhusiwa kushona nguo moja yake au ya ndungu wake wa karibu bila malipo ndani ya mwezi mmoja. Kabla ya mfanyakazi kushona nguo hiyo, ni lazima amjulishe meneja. Gharama za ushonaji wa nguo zisizidi shilingi elfu tano (TZS 5 000). Mfanyakazi analazimika kumpa meneja orodha ya gharama zitakazotumikishwa kwenye nguo. Kama kuna vitu ambavyo vitatumikishwa kwenye nguo ambavyo ofisi haina, mfanyakazi atajinunulia mwenye hivyo vitu.

8. Kila Jumatatu saa 17:30 hadi saa 19:00 mfanyakazi anaruhusiwa kutengeneza nguo zake zenye kuharibika, ila tu kama hizo nguo ni zake mwenyewe au za ndungu wake wa karibu. Kabla ya mfanyakazi kutengeneza nguo hizo, ni lazima amjulishe meneja. Gharama za utengenezaji wa nguo zisizidi shilingi elfu moja (TZS 1 000). Mfanyakazi analazimika kumpa meneja orodha ya gharama zitakazotumikishwa kwenye nguo. Kama kuna vitu ambavyo vitatumikishwa kwenye nguo ambavyo ofisi haina, mfanyakazi atajinunulia mwenye hivyo vitu.

9. Inakatazwa mfanyakazi kufanya kazi zingine zote zake za kibinafsi au za ndugu wake wa karibu ofisini. Ndungu wa karibu ni baba, mama, mke, mume, kaka, dada, mtoto, shangazi, mjomba, mjukuu, bibi, babu, mchumba na rafiki wa karibu. Mtu mwingine yeyote asiyetajwa hapa anahesabiwa kuwa ndugu yako wa karibu kama ni wewe ndiye unayechukuwa majukumu na malezi ya maisha yake, au kama munaishi pamoja. Mfanyakazi akitaka kuleta nguo zake au za ndugu wake wa karibu ofisini, zinapokelewa na kuhudumiwa kama nguo za wateja wengine. Kama inawezekana, mfanyakazi anayeleta nguo zake au za ndugu wake wa karibu asizishone mwenyewe. Zishonwe na wafanyakazi wengine. Kama ni vigumu wafanyakazi wengine kushona nguo za mfanyakazi mwenzao, mfanyakazi aliyeleta nguo zake au za ndugu wake wa karibu anaweza kuzishona mwenyewe kama meneja ataruhusu. Kama meneja hatoruhusu, ni lazima meneja atowe sababu halali.

10. Wanafunzi wanalipa shilingi elfu thelathini (TZS 30 000) kila mwezi. Malipo ya kwanza yanalipwa kabla ya kuanza kazi au kwenye tarehe ambayo mwanafunzi atahanza kazi. Mwanafunzi anasimamishwa ujifunzaji ikiheneya wiki mbili kamili za ukosefu wa kulipa malipo ya ujifunzaji baada ya tarehe iliyotakiwa malipo yafanyike. Mwanafunzi halipi malipo ya ujifunzaji kwenye siku ambazo amepewa likizo. Hii inamaanisha kuwa katika miezi ambayo mwanafunzi amepewa likizo, malipo hupunguzwa kulingana na siku ambazo alipewa likizo.

11. Bei ya ushonaji wa nguo inapangwa kwa namna hii: bei ya gharama za ushonaji wa nguo gawa kwa thelasini, halafu zidisha na mia. Mteja akibisha sana, bei inapangwa kwa namna hii: bei ya gharama za ushonaji wa nguo gawa kwa ishirini na tano, halafu zidisha na mia. Mteja akibisha tena, bei inapangwa kwa namna hii: bei ya gharama za ushonaji wa nguo gawa kwa ishirini na mbili, halafu zidisha na mia. Tunatumia bei kawaida za sokoni za vifaa tunapofanya hesabu za gharama.

12. Kama mteja ana nguo nyingi (tatu au zaidi), anapangiwa bei kwa namna hii: bei ya gharama za ushonaji wa nguo gawa kwa ishirini na tano, halafu zidisha na mia. Mteja akibisha sana, bei inapangwa kwa namna hii: bei ya gharama za ushonaji wa nguo gawa kwa ishirini, halafu zidisha na mia. Mteja akibisha tena, bei inapangwa kwa namna hii: bei ya gharama za ushonaji wa nguo gawa kwa kumi na nane, halafu zidisha na mia. Tunatumia bei kawaida za sokoni za vifaa tunapofanya hesabu za gharama.

13. Mteja atakeyeomba kwamba kazi za wateja wengine zisimamishwe ili kazi zake zifanyike kwa haraka, atalipa asilimia themanini juu ya bei ya kawaida. Mteja akibisha sana, anapunguziwa mpaka asilimia sitini na tano juu ya bei ya kawaida. Akibisha tena, anapunguziwa mpaka asilimia amsini juu ya bei ya kawaida. Kabla ya kufanya hesabu ya bei ya juu, tunafanya kwanza hesabu ya bei ya kawaida kwa namna hii: bei ya gharama za ushonaji wa nguo gawa kwa ishirini na tano, halafu zidisha na mia. Hesabu ya bei ya juu inafanyika kwa namna hii: bei ya kawaida gawa kwa mia, zidisha na asilimia uliokubalina na mteja kuhusu bei ya juu. Bei ya jumla inapatikana kwa namna hii: bei ya kawaida kujumlisha na bei ya juu. Tunatumia bei kawaida za sokoni za vifaa tunapofanya hesabu za gharama.

14. Kabla ya kuanza kazi ya ushonaji wa nguo za mteja, ni lazima mteja alipe angalau asilimia 30 ya bei ya malipo ya kazi. Malipo yatakayosalia lazima yalipwe ndani ya miezi 6 baada ya fundi kumaliza kushona nguo. Baada ya hii miezi sita, ofisi inaweza kuuza nguo za mteja. Ni ofisi ambayo inachukua pesa za mauzo.

15. Wafanyakazi wasiotumikia asilimia wanapata mshahara wao tarehe 1 kila mwezi. Wafanyakazi wote wanao tumikia asimilia, wanapata mshahara wao kwa makubaliano na meneja. Kama hakuna makubaliano yoyote yale kati ya meneja na wafanyakazi, meneja atawapa wafanyakazi wanaolipwa kwa asilimia mshahara mara mbili kwa mwezi. Tarehe 12 na tarehe 28. Siku moja kabla ya siku ya mshahara, meneja na kila mfanyakazi wanapaswa kuhakikisha pamoja ngapi mfanyakazi atapokeya.

16. Kila tarehe 15 ya mwezi, meneja anapaswa kutuma ripoti ya mwezi uliopita. Meneja uamua kile anachofikiri ni muhimu kuripoti, lakini ripoti inapaswa angalau kuwa na mada zifuatazo: 1. Idadi ya magizo. 2. Jina la kila fundi na idadi ya magizo aliyokamilisha. 3. Jumla ya mapato. 4. Jumla ya gharama / matumizi. 5. Maelezo ya matumizi ya fedha kwa kila gharama iliyozidi shilingi 5,000. 6. Jumla ya kiasi cha pesa kilichokopeshwa. 7. Jumla ya kiasi cha pesa za mikopo zilizolipwa. Ripoti ya meneja hutumwa kwenye barua pepe scaff@codinternational.com au kwenye WhatsApp +47 481 75 974. Ripoti inayotumwa kwenye WhatsApp inaweza ikawe ya maandishi au sauti.

17. Mbali na ofisi yenyewe, ofisi ina watu ambao hufanya kazi za uuzaji wa bidhaa za ofisi. Kila tarehe 15 ya mwezi, kila muuzaji anapaswa kutuma ripoti ya mwezi uliopita. Muuzaji uamua kile anachofikiri ni muhimu kuripoti, lakini ripoti inapaswa angalau kuzungumzia idadi ya nguo zilizouzwa na idadi ya nguo zilizobaki. Inakatazwa kukopesha nguo. Ripoti ya muuzaji hutumwa kwenye barua pepe scaff@codinternational.com au kwenye WhatsApp +47 481 75 974. Ripoti inayotumwa kwenye WhatsApp inaweza ikawe ya maandishi au sauti.

18. Ni marufuku kutumia / kugarimu pesa za kipato, yaani pesa za ushonaji, mafunzo au mauzaji. Kipato chote kitakuwa kinatumwa kwenye namba ya simu +255 713 672 338 (Kasibu Juma Msabaha). Kama kuna haja ya pesa za matumizi / gharama, tuma ombi kwenye WhatsApp + 47 481 75 974. Kabla ya kutuma pesa kwa Msahaba, ni lazima kuwasiliana naye kwanza.

19. Maadili yetu kwa kifupi: Tunahamasisha ushirikiano, ubunifu, upendo na mawazo huru katika kazi zetu. Tunawasiliana kwa uwazi, amani na uhalisia miongoni mwetu na wateja wetu.

20. Tutafanya kazi vizuri wakati mawasiliano ya wazi na ya kweli yanaheshimiwa na kuhimizwa. Ukijipata katika hali ngumu au inayokutia shaka, tunakuhimiza uzungumze na meneja. Ikiwa ni meneja ndiye chanzo cha tatizo, uzungumze na moja kati ya wamiliki. Ikiwa hujisikii huru kuzungumza na meneja au wamiliki, unaweza kupeleka kesi au tatizo lako kwa mwenye kiti au taasisi zingine zinazohusika na mambo ya sheria, haki, ushauri na uwamuzi.

21. Ikiwa utafahamu kuwepo kwa uvunjaji wa kanuni za kazi, sera, sheria au taratibu, unatakiwa kutaarifu meneja. Inakatazwa kubaki kimya ukifahamu kwamba kuna uvunjaji wa kanuni za kazi, sera, sheria au taratibu. Kubaki kimya kunakatazwa kwa sababu kunanyima fursa ya kutatua au kusuluhisha tatizo. Ikiwa ni meneja ndiye chanzo cha tatizo, uzungumze na moja kati ya wamiliki. Ikiwa hujisikii huru kuzungumza na meneja au wamiliki, unaweza kupeleka kesi au tatizo lako kwa mwenye kiti au taasisi zingine zinazohusika na mambo ya sheria, haki, ushauri na uwamuzi.

22. Mameneja na wasimamizi wana jukumu kubwa la kuongoza kwa mfano kwa kuwa na mienendo inayofuata kanuni, sera, sheria na taratibu zetu. Ikiwa wewe ni meneja au msimamizi, unatarajiwa:

kuhakikisha kwamba kila mfanyakazi aliye chini yako anajua na kuelewa kanuni, sera, sheria na taratibu husika, na jinsi ya kuzitumia.

kuonyesha kwa maneno na vitendo kujitolea kwako kufuata kanuni, sera, sheria na taratibu za kazi.

kuwahimiza wafanyakazi watafute ushauri au usaidizi bila woga wa kuadhibiwa au kisasi.

kuchukua hatua kwa haraka dhidi ya ukiukaji na changamoto zingine.

kukuza desturi ya kuzungumza kwa kuhakikisha kwamba kanuni, sera, sheria, taratibu na habari zingine za kazi zinajulikana na kupatikana kwa wafanyakazi wote.

23. Tunachukulia kila ripoti kwa uzito, tunachukua hatua haraka na kuchunguza kwa undani ikiwa ni muhimu. Sisi wote tunatakiwa kushirikiana kikamilifu katika uchunguzi wowote endapo tutaombwa kufanya hivyo. Katika hali kama hizo, ni sharti tutoe maelezo ya kweli na kamilifu.

24. Mazingira yetu yanafaa kuwa yanayowapa wafanyakazi wote ujasiri wa kuripoti matukio yoyote wanayojua au wanayoshuku kuwa hayafai au ya ukiukaji, na wafanye hivyo bila kuogopa kulipizwa kisasi. Inakatazwa kuchukuwa hatuwa yoyote mbaya au kulipiza kisasi dhidi ya mtu yeyote ambaye kwa nia njema ameripoti ukiukaji halisi au shaka ya ukiukaji.

25. Hatubagui wala kuwatendea wafanyakazi au wanao omba kazi kwa njia isiyo ya haki. Uamuzi wa kuajiri hufanywa kwa kuzingatia ustahili, kufuzu na utendakazi bila kuzingatia sifa nyingine kama vile kabila, rangi, dini, jinsia, taifa, usuli, uraia, umri, kuwa mwenye ulemavu, mwelekeo wa kimapenzi, utambulisho wa jinsia, hali ya kuwa mwanajeshi au mwanajeshi mstaafu na kuolewa au kutoolewa. Tunajituma kuhakikisha kwamba watu wenye sifa zinazotakikana wanaweza kukuza na kuendeleza ujuzi wao.

26. Kila mtu ana haki ya kufanya kazi katika mazingira yasiyo na unyanyasaji. Unyanyasaji ni tabia isiyofaa inayoathiri utendaji wa kazi au kufanya mazingira ya kazi yasiwe mazuri. Unyanyasaji unajumuisha kumwendea mtu kwa namna yoyote asiyotaka kupitia maneno, kumwangalia, kumgusa au udhalilishaji (uwe wa ngono au la) unachukiza au kufanya mazingira ya kazi yasiwe mazuri. Unyanyasaji hauruhusiwi kabisa. Ukiukaji utasababisha kuchukuliwa hatua za nidhamu, ikiwa ni pamoja na, kuachishwa kazi.

27. Ili kuhakikisha usalama wa kila mtu, kila mfanyakazi anatakiwa kuelewa na kufuata masharti na taratibu zote za usalama. Ukijua hali yoyote isiyo salama ya kufanyia kazi, unatakiwa kuripoti kwa meneja. Ikiwa ni meneja ndiye chanzo cha tatizo, uzungumze na moja kati ya wamiliki. Ikiwa hujisikii huru kuzungumza na meneja au wamiliki, unaweza kupeleka kesi au tatizo lako kwa mwenye kiti au taasisi zingine zinazohusika na mambo ya sheria, haki, ushauri na uwamuzi.

28. Haturuhusu kuwa na silaha mahali pa kazi. Haturuhusu pia vitendo au vitisho vya ghasia. Wafanyakazi wanatakiwa kuripoti mara moja kwa meneja vitisho au hofu ya ghasia. Ikiwa ni meneja ndiye chanzo cha tatizo, uzungumze na moja kati ya wamiliki. Ikiwa hujisikii huru kuzungumza na meneja au wamiliki, unaweza kupeleka kesi au tatizo lako kwa mwenye kiti au taasisi zingine zinazohusika na mambo ya sheria, haki, ushauri na uwamuzi.

29. Kufanya kazi ukiwa umelewa dawa za kulevya au pombe kunasababisha mazingira hatari isiyokubalika kwako na wengine. Tukiwa wafanyakazi, haturuhusiwi kuwa na, kutumia au kufanya kazi tukiwa tumelewa pombe au dawa zingine za kulevya. Wafanyakazi hawaruhusiwi kutenda majukumu yao wakiwa wametumia dawa zozote zinazoweza kuathiri utendaji wao wa kazi au kuwa hatari kwa usalama.

30. Wafanyakazi ambao wamejeruhiwa na vifaa vya kazi wakati wa kazi, hulipiwa gharama za matibabu na mwajiri. Gharama ambazo hugharamiwa na mwajiri ni gharama ambazo hazilipwi na sherikali, vitengo vingine, shirika zingine au watu wengine. Mwajiri hachukui jukumu la majeraha na magonjwa ambayo hayatokani na kazi, hata ikiwa jeraha au ugonjwa umetokea wakati wa saa za kazi. Ila ikiwa umekuwa mgonjwa sana na hauwezi kwenda nyumbani, hospitalini au kwa daktari peke yako, mwajiri atalipa gharama za kukufikisha nyumbani, hospitalini au kwa daktari hata kama ungonjwa ahukusababishwa na kazi.

31. Ikiwa itabidi ukae nyumbani kwa sababu ya jeraha au ugonjwa uliopata kwa sababu ya kazi wakati wa kazi, utapokea mshahara kwa miezi tatu. Mshahara utakaopokea ni mshahara wa mwezi wa mwisho uliokamilika kabla ya jeraha. Kwa kuipata haki ya kupata mshahara huu, ni lazima daktari aandike kithibitisho kwamba ni lazima uwe nyumbani kwa sababu ya jeraha. Kwa kithibitisho, daktari lazima aeleze ni kwa muda gani unapaswa kuwa nyumbani.

32. Sote tuna jukumu sawa la kulinda na kutumia vizuri mali na vifaa vya kazi ili kuzuia hasara, uharibifu, wizi na matumizi mabaya. Mali na vifaa halisi ni pamoja na majengo, bidhaa, fedha, simu, chereani, vifaa na vitu vingine vya kazi. Kila mfanyakazi anatarajiwa kuwa mlinzi mwema wa mali na vifaa kwa kuvitumia kwa ubora na kuvilinda dhidi ya matumizi yasiyoidhinishwa.

33. Katika kipindi ambacho umeajiriwa unaweza kupata taarifa fulani kuhusu kazi, wateja au washirika ambayo ni ya faragha au ya kikazi. Taarifa za faragha zinajumuisha maelezo yoyote yasiyopatikana kwa umma ambayo yanaweza kutumiwa na washindani wetu, au ambayo yakifichuliwa, ni hatari kwa kazi au wateja. Unafaa kuchukulia taarifa za kazi na wateja kuwa faragha kila wakati isipokuwa kama una uelewa wa waziwazi kwamba maelezo hayo yanapatikana kwa umma. Ni sharti uchukuwe tahadhari inayofaa kila wakati kulinda taarifa za faragha ambazo unazopata.

34. Ingawa tabia ya kutoa na kupokea zawadi inaweza kukuza uhusiano bora wa kazi, kuna uwezekano wa kuwa iwe na mgongano wa maslahi au kuonekana kuwa na mgongano. Kwa sababu hiyo, tunajukumu la kuhakikisha kwamba zawadi au burudani yoyote inayotolewa au kupokelewa inaruhusiwa na kanuni zetu na sera au sheria zozote husika. Haturuhusiwi kabisa kutoa au kupokea zawadi au burudani yoyote, iwe ni moja kwa moja au kupitia watu wengine kwa lengo la kushawishi uamuzi katika kazi au kuathiri uwezo wa kufanya uamuzi huru. Zawadi yoyote tunayotoa au kupokea katika mahusiano ya kikazi haifai kuwa na thamani ya kifedha. Isiwe pia ya mara kwa mara. Mfano wa zawadi ambayo ina thamani ya kifedha ni alimasi. Mifano ya zawadi zinazokubalika ni zawadi ambazo ofisi imewapa wafanya kazi wote, mauwa na chakula ndogo. Zawadi zisizokubalika ni kama zawadi za pesa au sawa na pesa, zawadi inayotolewa ili kupokea faida ya binafsi au ushawishi kwenye kazi, zawadi zinazokiuka sheria, zawadi na burudani za ngono au zawadi zinazokiuka maadili yetu, na zawadi kwa maofisi za serikali.

35. Kuzuia, kutambua na kuripoti rushwa na ufisadi ni jukumu la kila mfanyakazi. Tunataka kudumisha imani kati yetu na wateja, pia na washirika wetu. Imani hiyo inapatikana kwa ubora ikiwa sisi sote tutafanya shughuli zetu kwa kuzingatia maadili na uaminifu. Huwa hatuamui kushiriki rushwa au tabia nyingine za ufisadi. Hatutoi wala kupokea rushwa. Hatuombi wala kukubali rushwa. Hatufanyi malipo ya kulainisha mambo au kuwaruhusu watu wengine wafanye hivyo kwa niaba yetu.

36. Wafanyakazi hujikuta wakiulizwa maswali kuhusu kazi zetu na watu wa nje. Mfano; wahandishi wa habari au watu wa ofisi za serikali. Wafanyakazi walioteuliwa tu (wamaneja na mafundi wakuu kwa mfano) pekee ndio wanaoweza kujibu maombi na maswali hayo. Wakati wa mawasiliano ya nje ni lazima kuhakikisha kwamba ujumbe unaowasilishwa umeandaliwa vizuri ukiwa na taarifa sahihi.

Ilisasishwa mwisho: 29.06.2022
Inatumika kutoka: 01.07.2022